Pakua Faili la PDF
Maelezo
Yeye ni Mtume aliyetumwa kwa watu wote na yeye ndie Mtume wa mwisho na yeye ndio kiongozi wa mitume, amekuja na dini ya uislamu ambayo hatakubali Mwenyezi Mungu Siku Ya Kiyama dini yeyote isipokuwa uislamu. Yeye amezaliwa katika kabila la Qureysh kabila tukufu katika mji wa Maka. Mtume ametokana katika ukoo wa Ibn Hashimu. Na ukoo huu umeitwa kwa jina hili kutokana na kurithi jina hili kutoka kwa mzee wao Hashim Ibn Abd Manaf. Mtume (s.a.w) alizaliwa siku ya juma tatu katika mweze rabil-awali (mfunguo sita) mwezi tisa (9) kwa mujibu wa wanahistoria katika mwaka wa tembo 571 B.K. baada ya kuzaliwa mama yake alituma mtu aende akatoe habari kwa mzee Abdul al-Muttalib juu ya kuzaliwa kwa mtoto. Kwa furaha kabisa alikuja mzee na akamchukuwa mtoto akambeba na kuelekea nae mbele za al-ka’aba (nymba tukufu ya Allah) kwa kutoa shukrani zake za dhati kwa Mwenyezi Mungu. Kisha akampa jina la Muhammad, jina ambalo halikuwa likijulikana na waarabu.
Maudhui ya kozi
Jumla : 10 Mihadhara
Mwalimu wa kozi
Sehemu
- Muda Uliokadiriwa: 87 dakika
- Mihadhara 10
-
Lugha
Kiswahili
- Maswali 10
- Kuonyesha masomo 0
- Kiwango cha ujuzi Beginner
- Wanafunzi 1,940