UBORA WA UISLAMU

UBORA WA UISLAMU

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na Mwenye kutafuta dini isiyokuwa dini ya Kiislamu, ambayo ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kumpwekesha na kumfuata kwa kumtii na kumdhalilikia, na kwa Mtume wake aliye Nabii wa mwisho Muhammad, Rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwa kumuamini na kumfuata na kumpenda kwa dhahiri na kwa siri, basi […]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na Mwenye kutafuta dini
isiyokuwa dini ya Kiislamu, ambayo ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa
kumpwekesha na kumfuata kwa kumtii na kumdhalilikia, na kwa Mtume wake
aliye Nabii wa mwisho Muhammad, Rehema za Mwenyezi Mungu na amani
zimshukie, kwa kumuamini na kumfuata na kumpenda kwa dhahiri na kwa siri,
basi hiyo haitakubaliwa kwake, na yeye Akhera atakuwa ni miongoni mwa
wenye kupata hasara ambao walizifanyia ubahili nafsi zao kwa kuzinyima
mambo yenye kuzinufaisha”. [Al-Imran: 85]. Na kauli ya Allah Mtukufu:
«Na miongoni mwa mambo aliyowausia Mwenyezi Mungu ni kwamba huu
Uislamu ndio njia ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, iliyolingana sawa. Basi
ifuateni wala msifuate njia za upotevu zikawatawanya na kuwaepusha na njia
ya Mwenyezi Mungu iliyolingana sawa. Muelekeo huo upande wa njia nyoofu,
ndio Aliowausia nao Mwenyezi Mungu ili mjikinge na adhabu yake kwa
kuyatekeleza maamrisho yake na kijitenga na makatazo yake.» (Al-An’am)
Amesema Mujaahidi: neno Al- subulu: maana yake ni Uzushi na
mambo yenye kutatiza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *